FEATURED POST

Loeb atisha hatua ya nane, Al-Attiyah ajikusanyia pointi za jumla Dakar Rally 2019

Dereva wa magari raia wa Qatar Nasser Al Attiyah amezidi kuchanja mbuga kwa kujiongezea alama kwenye mbio za Dakar Rally mwaka huu huku S...

Sunday, 22 April 2018

LEO KATIKA HISTORIA: Kifo cha Bondia Rubin ‘Hurricane’ Carter

Rubin 'Hurricane' Carter

Aprili 20, 2014 alifariki dunia mwanamasumbwi wa uzito wa kati Rubin ‘Hurricane’ Carter. Mpiganaji huyo wa ulingoni nchini Marekani alifariki dunia akiwa na miaka 76.

Akifahamika zaidi kama Hurricane kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao ulingoni akitumia mapigo ya orthodox. Hurricane aliweka rekodi ya kucheza mapigano 40 akishinda 27 katika hao alishinda kwa KO mapigano 19, alipoteza mapigano 12 na kutoka sare pambano moja tu. Nyota huyo alikuwa na kimo cha mita 1.73 ambapo alikuwa mfupi na viwango vya urefu kwa wapambanaji wa uzito wa kati. Lakini alisalia kupambana katika uzito wa kilo kati ya 70 na 72.6; hata hivyo kutokana na mtindo wake wa kuingia kwa nguvu bila kumuachia nafasi mpinzani wake kulimfanya awe maarufu.

Halafu usiombe konde lake likukute, hakika lilikuwa na uzito ambao utamlewesha mpinzani hali iliyokuwa ikimpa ushindi kwa KO ya mapema. Mashabiki ndio waliompa jina la Hurricane baada ya kuwakung’uta mabondia wa uzito wa kati kama Florentino Fernandez, Holley Mims, Gomeo Brennan na George Benton. Julai 1963 jarida la Ring lilimtaja katika orodha ya mabondia bora 10, haikuishia hapo mwaka 1965 Hurricane alipanda chati katika jarida hilo na kuwa miongoni mwa mabondia watano bora wa uzito wa kati.

Atakumbukwa katika matukio mengi lakini mojawapo ni la kutupwa jela ambako alitumikia miaka 20. Alizaliwa Juni 6, 1937. Hurricane alitupwa jela kimakosa baada ya kupatikana na makosa ya kuua. Mwaka 1966 alikamatwa na polisi akiwa na rafiki yake John Artis wakati huo alikuwa akishikilia mkanda wa uzito wa kati wakihusishwa na tukio la mauaji katika baa ya Lafayette na Grill mjini Paterson, New Jersey. Baada ya hapo walihusishwa na matukio mengine yalikuja kutokea mwaka 1967 na 1976. Hurricane alitupwa katika jela ya Rahway State.

Aliachiwa mwaka 1985. Tangu mwaka 1993 hadi 2005 alikuwa  akikitumikia Chama cha Ulinzi kwa watu wanaosingiziwa makosa. Machi 2012 wakati akihudhuria Kongamano la Kimataifa la Haki mjini Burswood, Western Australia; Hurricane aliweka bayana kuwa ana maradhi ya saratani ya kizazi.

Kwa wakati huo madaktari walikaririwa wakisema atakuwa na miezi isiyozidi sita ya kuishi. Tangu wakati huo rafiki yake wa kitambo John Artis alisalia kuwa mhudumu wake, na Aprili 20, 2014 alithibitisha kuwa rafiki yake aliyekuwa akimhudumia amefariki dunia. Miezi miwili kabla ya kifo chake Hurricane aliandika mtazamo katika Gazeti la New York Daily News iliyopewa jina la “Hurricane Carter’s Dying Wish” akidai haki yake mahakamani kuhusu David McCallum akitaka mahakama imsafishe. Oktoba 15, 2014 McCallum alisafishwa na mahakama kuwa hakuwa na hatia.

No comments:

Post a Comment