Merry Christmas 2015

Pamoja kwa Umoja

Friday, April 21, 2017

Aprili 22, 2015


John Moshoue

Aprili 22, 2015 alifariki kocha wa zamani wa Afrika Kusini John Moshoue. Kocha huyo aliwahi kuwa mchezaji wa zamani wa Kaizer Chiefs na klabu ya Fenerbahce  ya Uturuki. 

Alifariki dunia katika Hospitali ya Morningside baada ya kupigania uhai dhidi ya saratani ya tumbo. Kabla ya kifo chake alipelekwa katika Hospitali ya Charlotte Maxeke. Ibada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa la Grace Bible lililopo Soweto na kuzikwa katikamakaburi ya Westpark yaliyopo Randburg Aprili 27, 2015. 

Katika maisha yake ya soka akiwa na timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana yalikuwa hivi. Alikuwa miongoni mwa kikosi kilichotwaa taji la Mataifa ya Afrika mwaka 1996 akimaliza wa pili kwa ufungaji wa mabao kwenye michuano hiyo akifumania nyavuu mara nne. Pia alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Bafana Bafana kilichoitwaa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini Ufaransa. 

Aidha Moshoue alishiriki katika michuano sita ya kimataifa akiwa na Bafana Bafana. Hadi anastaafu kuhudumu katika kikosi cha taifa hilo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa. Mechi hiyo ilikuwa dhidi ya Nigeria iliyochezwa Monastir nchini Tunisia Machi 31, 2004 akiwa na miaka 38, mwezi mmoja na siku 13 alicheza mtanange huo, hivyo kuweka rekodi ya mechi 73 na mabao 8 huku akianza mechi 68. 

Pia atakumbukwa kwa bao lake dhidi ya Botswana Januari 10, 1993  alilofunga akiwa na Bafana Bafana akitoka majeruhi ya miezi sita baada ya kuvunjika mguu na kukaa nje kwa miezi sita lilimpa ari ya kuendelea kuhudumu kwenye kikosi hicho. Enzi zake za uchezaji Mohoue alikuwa akifahamika na mashabiki, alizaliwa Ga Mashashane, Limpopo Desemba 18, 1965 na kukulia Diepkloof, Soweto. 

Alishawahi kuzitumia Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, AmaZulu. Alitua nchini Uturuki baada ya wakala wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Marcelo Houseman kuanzia 1997-2001 akicheza mechi 75 na kufunga mabao 15 akiwa na Fenerbahce. Alisalia Uturuki katika klabu Bursapor alikocheza mechi 48 na kufunga mabao saba. 

Pia Moshoue aliwahi kunolewa na Wajerumani Franz Beckenbauer na kocha wa sasa wa Ujerumani Joachim Low.

No comments:

Post a Comment

Jabir Johnson at Mkalama, Singida on 25 May 2016

Jabir Johnson at Mkalama, Singida on 25 May 2016

Jabir Johnson at Msolwa Sec. School

Jabir Johnson at Msolwa Sec. School
It was 28th May 2016

Jabir Johnson (The Journalist)

Ligi Kuu za Kandanda

Ligi Kuu za Kandanda

Jabir Johnson at BWM Stadium

Jabir Johnson Mking'imle

Jabir Johnson in Dar es Salaam

Jabir Johnson in Dar es Salaam

UCL 2015/16

Cristiano Ronaldo

Lake Victoria source of River Nile

Lake Victoria source of River Nile
Jabir Johnson at source of River Nile, Lake Victoria on May 21, 2016
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

G


website counters

TOPSy KRETTS

Followers