Merry Christmas 2015

Pamoja kwa Umoja

Sunday, April 22, 2018

LEO KATIKA HISTORIA: Kifo cha Bondia Rubin ‘Hurricane’ Carter

Rubin 'Hurricane' Carter

Aprili 20, 2014 alifariki dunia mwanamasumbwi wa uzito wa kati Rubin ‘Hurricane’ Carter. Mpiganaji huyo wa ulingoni nchini Marekani alifariki dunia akiwa na miaka 76.

Akifahamika zaidi kama Hurricane kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao ulingoni akitumia mapigo ya orthodox. Hurricane aliweka rekodi ya kucheza mapigano 40 akishinda 27 katika hao alishinda kwa KO mapigano 19, alipoteza mapigano 12 na kutoka sare pambano moja tu. Nyota huyo alikuwa na kimo cha mita 1.73 ambapo alikuwa mfupi na viwango vya urefu kwa wapambanaji wa uzito wa kati. Lakini alisalia kupambana katika uzito wa kilo kati ya 70 na 72.6; hata hivyo kutokana na mtindo wake wa kuingia kwa nguvu bila kumuachia nafasi mpinzani wake kulimfanya awe maarufu.

Halafu usiombe konde lake likukute, hakika lilikuwa na uzito ambao utamlewesha mpinzani hali iliyokuwa ikimpa ushindi kwa KO ya mapema. Mashabiki ndio waliompa jina la Hurricane baada ya kuwakung’uta mabondia wa uzito wa kati kama Florentino Fernandez, Holley Mims, Gomeo Brennan na George Benton. Julai 1963 jarida la Ring lilimtaja katika orodha ya mabondia bora 10, haikuishia hapo mwaka 1965 Hurricane alipanda chati katika jarida hilo na kuwa miongoni mwa mabondia watano bora wa uzito wa kati.

Atakumbukwa katika matukio mengi lakini mojawapo ni la kutupwa jela ambako alitumikia miaka 20. Alizaliwa Juni 6, 1937. Hurricane alitupwa jela kimakosa baada ya kupatikana na makosa ya kuua. Mwaka 1966 alikamatwa na polisi akiwa na rafiki yake John Artis wakati huo alikuwa akishikilia mkanda wa uzito wa kati wakihusishwa na tukio la mauaji katika baa ya Lafayette na Grill mjini Paterson, New Jersey. Baada ya hapo walihusishwa na matukio mengine yalikuja kutokea mwaka 1967 na 1976. Hurricane alitupwa katika jela ya Rahway State.

Aliachiwa mwaka 1985. Tangu mwaka 1993 hadi 2005 alikuwa  akikitumikia Chama cha Ulinzi kwa watu wanaosingiziwa makosa. Machi 2012 wakati akihudhuria Kongamano la Kimataifa la Haki mjini Burswood, Western Australia; Hurricane aliweka bayana kuwa ana maradhi ya saratani ya kizazi.

Kwa wakati huo madaktari walikaririwa wakisema atakuwa na miezi isiyozidi sita ya kuishi. Tangu wakati huo rafiki yake wa kitambo John Artis alisalia kuwa mhudumu wake, na Aprili 20, 2014 alithibitisha kuwa rafiki yake aliyekuwa akimhudumia amefariki dunia. Miezi miwili kabla ya kifo chake Hurricane aliandika mtazamo katika Gazeti la New York Daily News iliyopewa jina la “Hurricane Carter’s Dying Wish” akidai haki yake mahakamani kuhusu David McCallum akitaka mahakama imsafishe. Oktoba 15, 2014 McCallum alisafishwa na mahakama kuwa hakuwa na hatia.

Tuesday, April 17, 2018

LEO KATIKA HISTORIA: Rekodi ya Kwanza ya Watazamaji wengi katika Soka yawekwa


Uwanja wa Hampden Park jijini Glasgow, Uskochi mwaka 1937
Aprili 17, 1937 Timu ya Soka ya Scotland iliwakaribisha mahasimu wao England katika dimba la Hampden Park ikiwa ni michuano ya nyumbani ya Waingereza mwaka huo.

Kinachokumbukwa katika mchezo huo ni umati wa watazamaji waliofurika kuutazama mtanange ambapo ilirekodiwa watazamaji 149,415. Rekodi hiyo ilisalia wakati huo hata Guiness Record waliirekodi kuwa imevunja rekodi zote katika soka duniani. Takwimu hiyo inasalia kuwa kubwa kwa michuano ya Ulaya kuwahi kutokea.

Siku ya mchezo huu, mahasimu hao walikuwa wakiwania nafasi ya pili baada ya Wales kuwa tayari imeshatwaa taji hilo kwa kushinda michezo yote mitatu. Scotland na England zilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Wales, na Wales walishinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Ireland. Siku hiyo Mshambuliaji wa Uskochi Bob McPhail aliifungia timu yake mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya England.

Ikumbukwe rekodi halisi ya watu haijulikani kwani inaonyesha idadi kubwa ya watu walioingia uwanjani hawakulipa viingilio, Lakini iliyorekodiwa ni 149,415. Hata hivyo rekodi hiyo licha ya kurekodiwa na vyanzo mbalimbali ilikuja kuvunjwa mwaka 1950 katika mchezo wa Kombe la Dunia baina ya Uruguay na Brazil kwenye dimba la Maracana jijini Rio de Janeiro.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), linasema idadi ya mchezo huo wa fainali jijini Rio, ilikuwa 173,850 lakini inasemekana wengi waliingia kinyume cha sheria ambao rekodi yao haikuingizwa katika takwimu hizo. Hata hivyo rekodi ya mwaka 1937 inasalia kuwa ya pekee katika michuano ya soka barani Ulayani.

HAPPY BIRTHDAY: Ramadhani Hassan Milambo

I wish you all the best, you are true friend of mine. In troublesome and joyful moments you were with me. You are human being. God be with you all the way long; Ramadhani Hassan Milambo a.k.a Norman. Kufikisha miaka 30 sio jambo dogo, ni Mwenyezi Mungu Aliyezifanya Mbingu na Nchi wa kutukuzwa. No matter what.

Tuesday, April 10, 2018

LEO KATIKA HISTORIA: Genoa FC yaanzishwa

Aprili 10
Mabadiliko katika jambo lolote lile hayapingiki kutokana na kubadilika kwa nyakati. Soka limepitia mabadiliko mengi katika maeneo tofauti hapa ulimwengu.

Genoa FC
Aprili 10, 1897 Klabu ya Kriketi na Riadha ya Genoa nchini Italia ilipanua wigo wake na kuongeza mchezo wa soka. Historia hiyo inadumu hadi leo ya kuifanya Genoa kuwa klabu ya zamani ya soka iliyo hai nchini humo. Kwa wakti huo kuliko na klabu nyingine za soka Turin-Internazionale Torino na ile ya FCB Torinese.

Genoa ilianzishwa mwaka 1893 na Waingereza waliohamia katika ardhi hiyo, ambao walijikita katika mchezo wa kriketi huku wakiuchukulia mchezo wa soka kuwa ni wa watu wa chini na sio kwa wale wenye uwezo wa kimaisha. Lakini mwaka 1897 James Richardson Spansely ambaye alikuwa daktari wa Uingereza na mpenzi wa soka aliwashawishi wenzake kuwa na idara ya soka.

Hivyo kwa kuanza alianza kuwa meneja wa timu hiyo. Genoa ilianza kupata mafanikio kwa kutwaa taji la kwanza la Italia mwaka 1898 na kuanzia hapo ilishinda mataji matano yaliyofuata kati ya sita ikipoteza mwaka 1901 dhidi ya Milan.

Baada ya hapo Internazionale Torino ilipotea mwaka 1900 na mwaka 1906 Torinese ilifuata hivyo kuiacha Genoa hadi sasa. Kwa ujumla Genoa imetwaa mataji tisa ya Skudetto. Pia ilitwaa Kikombe cha Italia mwaka 1937 na kile cha Anglo-Italia mwaka 1996.

Monday, March 26, 2018

MTAZAMO: Tanzania Tumerogwa?


NA JABIR JOHNSON
johnsonjabir@gmail.com
+255-(0)-768 096 793
Alfajiri ya Februari 22, mwaka huu Tanzania ilipokea ugeni mkubwa katika soka. Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino na ujumbe wake walikanyaga ardhi yetu na kulakiwa na viongozi wa Serikali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Michael Wambura na Wales Karia katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mjini Dodoma. CHANZO: Sufiani Mafoto
 
 Jambo hilo halitasahaulika katika matukio ya mwaka huu kwani ni bahati njema. Infantino mwenye asili ya Uswisi na Italia aliisifia sana Tanzania kuwa ni nchi ya soka, ya watu wanaopenda soka.

Akizungumzia jitihada za kukuza soka barani Afrika, Infantino alielezea kuwa siku za nyuma Afrika ilikuwa inapata dola za kimarekani milioni 26 kutoka Fifa, lakini sasa hivi, Afrika inapata dola za kimarekani milioni 100 ili kuiinua mchezo wa soka.

Pamoja na hayo alisema katika kipindi chake amejaribu kuhakikisha ongezeko la timu za Afrika katika kushiriki michuano ya kombe la dunia .

Tangu aingie madarakani, Rais huyo wa Fifa aliongeza idadi ya timu zitazoshiriki michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2026 toka 5 mpaka 7. Infantino akaagwa kwa mbwembwe baada ya mkutano huo.

Hata mwezi mmoja haujamalizika tayari huko TFF kimeshanuka, Makamu wa Rais Michael Wambura amefungiwa maisha kujihusisha na masuala ya michezo akihususishwa na makosa matatu ya kimaadili katika shirikisho hilo.

Makosa hayo ni kupokea  fedha isiyo halali kinyume cha Kifungu cha 73(1) cha kanuni za maadili za TFF Toleo la 2013. Kosa jingine ni kughushi barua ya kueleza alipwe malipo Kampuni ya Jecks System Limited huku akijua malipo hayo sio halali pia kosa la tatu ni kushusha hadhi ya shirikisho hilo.

Ilielezwa malipo hayo ya kughushi yalifanyika Juni 21, 2016 ambapo mke wa marehemu ambaye alikuwa mmoja wa wakurugenzi  Irene Maganga, Kampuni hiyo ilikanusha  kupokea fedha hizo kutoka TFF.

Mengi yalijiri katika kikao hicho kilichofikia mwafaka wa kumfungia maisha Wambura. Kinachostaajabisha ambacho kwa sasa nasema bila hofu yoyote ni kwamba ‘Tanzania Tumerogwa na mchawi mwenyewe alishajifia bila kutegua tego lake’.

Tunataka kuirudisha TFF ya migogoro ambayo itakuwa haina tija, halafu ni aibu taarifa zirudi Fifa kuwa Infantino baada ya kuondoka, shirikisho limeingia katika sintofahamu.
Halafu imeonekana kama kitu ni rahisi kumfungia mtu maisha asishiriki michezo. Lakini ninachokiona Wambura anapaswa afikishwe mahakamani kabisa akajieleze huko hususani kosa lake la kughushi kwani ni kinyume hata na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aende jela. Si ndio tunataka iwe hivyo.

Uchaguzi ulishafanyika na kuwaingiza madarakani, lakini kinachoonekana ni bifu za chini kwa chini ambazo ni hatari kwa soka la Tanzania ambalo tutavuruga kila kitu na kuwa taifa mfu. 

Jamani waoneeni huruma mashabiki wa soka wa Tanzania ambao nao wanatamani siku moja timu ya Taifa icheze Kombe la Dunia na klabu nchini ziishiriki michuano ya kimataifa katika hatua za juu kama zilivyo Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Bayern Munich na nyingine nyingi.

Sasa mnatukumbusha yaliyotokea enzi za FAT, hii ni hatari kwanini msifute na kuanza upya sasa ona kosa la mwaka 2016 hata kabla Rais wa TFF Karia hujaingia madaraka. Hapo kuna namna ambayo sio nzuri katika maendeleo ya soka.

Wapenda soka nchini walianza kuwa na imani na TFF lakini mnaanza kuharibu kutokana na matakwa binafsi, hapo naona wazi matakwa ya wachache ndio shinikizo kubwa la sakata hili. Kwanini pingamizi lisingeletwa wakati wa kinyang’anyiro cha nafasi ya Makamu wa Rais uliomweka madarakani Wambura. 

Hapa ndipo napokubaliana na wale wanaosema akili za watu wenye ngozi nyeusi ni ndogo kupita maelezo, lakini hayo yote tunayataka wenyewe. Siku wenye ngozi nyeupe watakapokuja kutuamulia tunaanza kuona kama Mwenyezi Mungu aliwapendelea, na sisi ndio tumerogwa?

Saturday, March 3, 2018

Mfahamu Ally Bakari Ali 'Ally B' wa Kijitonyama United FC

Ally B akiwa na Kijitonyama United FC mwaka 2018
 katika Uwanja wa Shule ya Msingi 
Mwananyamala B, jijini Dar es Salaam
Katika michezo kuna wanamichezo wakubwa na makocha ambao hakika utapenda wakati wote kusikia kitu kutoka kwao kuhusu michezo.
Unaposikia majina ya nyota wakubwa kama Muhammad Ali, Michael Jordan, Babe Ruth, Vince Lombardi, John Wooden na wengine wa kizazi cha leo kama Lebron James, Arnold Schwarzenegger, Cristian Ronaldo, Lionnel Messi, Roger Federer basi kuna hutaacha kutega sikio kwa sekunde kadhaa ili ujue kuna nini kinachozungumzwa kwao.
Hali hiyo imewafanya hata vijana wanapochipukia katika michezo hapa nchini nao kuamini kwamba ipo siku moja watakuwa juu. Ndio sababu siku moja mkali wa zamani katika mchezo wa Baseboli hapa ulimwenguni Babe Ruth alisema, “Ni vigumu sana kumshinda mtu ambaye hakati tamaa.”
Kauli hiyo inaweza kuwa miongoni mwa chachu inayomtia nguvu mchezaji wa kandanda anayeishi katika mitaa ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam Ally Bakari Ali.

Kwanini Ally Bakari Ali?
Katika mitaa ya Kijitonyama ambako alikulia kijana huyo mwenye kimo cha yapata futi tano na inchi kadhaa hivi hufahamika sana kwa jina la ‘Ally B’.
Hiyo inatokana na umahiri wake wa kusakata kabumbu katika nafasi ya kiungo wa kati, huku macho ya wengi yakisalia kufurahia burudani kutoka kwa nyota huyo anayerandaranda bila msaada wowote wa kufikia kucheza kama mchezaji mkubwa wa baadaye.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii anasema, “Ninaendelea kutafuta channel za kuniwezesha kutoboa, hata hivyo mapito ni magumu ila naamini ndoto zangu za kucheza soka nje ya Tanzania zitatimia.”
Unyumbufu wa viungo vyake pindi akishika mpira ndio utapenda na unaweza kusema amewekewa ‘spring’ zinazomfanya awe hivyo lakini utasalia kusema ni kipaji alichokirimiwa na Mwenyezi Mungu.

Ally B akiwa nyumbani kwao Kijitonyama United FC

Changamoto katika Ndoto zake
Ally B
Knute Rockne (1888-1931) ambaye ni miongoni mwa makocha maarufu katika mchezo wa American Football hapa duniani aliwahi kusema katika hotuba zake kwa wachezaji, “Mtu mmoja anayeshiriki michezo yuko mbali zaidi kuliko anayehubiri michezo.”
Wakati anazungumza hayo alikuwa akijua wazi kuwa katika kushiriki kucheza kuna changamoto ambazo atakutana nazo mchezaji husika. Hivyo ndivyo kwa Ally B tangu alipoingia katika kandanda amekutana na changamoto lukuki
 “Kwanza wazazi awali ilikuwa shida kunielewa nini nafanya kwenye soka lakini baadaye walikuja kuelewa, lakini katika timu nilizopitia migogoro ya viongozi imekuwa ikinirudisha nyuma,” anasema Ally B.
Mbali na changamoto hizo Ally B anasema ujio wa wachezaji wapya katika timu umekuwa ukichangia kiwango chake kutoimarika katika mazingira ya Kitanzania yalivyo pia mbinu za ufundishaji za walimu  zimekuwa mwiba mkali kwani walimu wengine wameshindwa kumwamini kabisa kwamba anaweza kufanya mambo makubwa dimbani.

Undani kuhusu Maisha yake
Ally B ana asili ya Pemba huko visiwani Zanzibar, katika kabila la Washirazi. Alizaliwa Juni 6, 1997 Mwananyamala jijini Dar es Salaama kwa wazazi Bakari Ali Msuri na Raya Yusuf Mkwaju.
Nyota huyo ni wa tatu katika familia yao ya watoto wanne. Alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Kijitonyama na kuhitimu mwaka 2010 kisha elimu ya upili (sekondari) katika shule ya Makumbusho kati ya mwaka 2011-2014.
Baada ya masomo hayo ndoto zake hadi sasa ni kucheza kandanda. Alianza na timu ya watoto ya Kijitonyama Kisiwani mwaka 2012 ilipofika mwaka 2014 aliingizwa katika timu ya wakubwa ya Kijitonyama Chipukizi ambako alidumu hadi mwaka 2017.
Msimu wa 2015/16 Ally B alipata fursa ya kucheza Ligi Daraja la Nne na mwaka 2017 alishiriki Kikombe cha Chipukizi chini ya Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA).
Kwa sasa anaitumikia klabu ya Ligi Daraja la Pili Ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam Kijitonyama United ambayo inapambana kuingia katika Ngazi ya Taifa.

Ally B akizungumza na Ramadhani Hassan Milambo
Imeandikwa na Jabir Johnson, Februari 2018.

Thursday, December 28, 2017

Amateur Soccer Records of Jabir Johnson in 2017


My motto of 2017: Be so busy improving yourself. You have no time to criticize others.

Matches Played: 54
Game Analysis: P54 W20 L19 D15
Minutes Covered: 2929
Position Played: Full Backs, Wings, Forward, Centre Backs
Teams Played: Taswa FC, Kijitonyama, Tandale Veterans, 5Star, New Champion, Sahara Media Group, Combine Bay Street-Mwananyamala.

Goals Scored: 3
Assists: 5
Contribution: 12
Yellow Card: 1
Red Card: 0

Position played Most: Full Backs (26 games)
Position played Less:Centre Backs (6 games)
Games started: 37
Games from subs: 17

Matches by Position
Forward: 12
Wings: 10
Full Backs: 26
Centre Backs: 6

Matches by Teams
Taswa FC: 11
Kijitonyama: 15
Tandale Veterans: 17
Sahara Media Group: 6
5Star : 2
New Champion: 1
Combine Bahi Street: 2

Most goals per game: Boko FC 5-4 Kijitonyama, 8/10/2017 Boko Primary School ground.
Most Win: Polisi FC 0-5 Taswa FC, 4/11/2017 Uhuru Stadium-Temeke.
Most Defeat: Kijitonyama 0-5 Lugalo JWTZ, 27/8/2017 ISW-Ustawi.

If you don’t want to practice, you don’t really want to win.


Monday, November 20, 2017

Nana Baby ‘Promising Talent’ la Bongo Fleva

Tangu Oktoba 2017 Jaizmelaleo ilianza kukuletea ukurasa wa mbele wa jarida lake la JAIZMELALEO.  

Matthew McColister kocha wa kikapu nchini Marekani aliupamba ukurasa wa huo. Novemba hii anayeupamba ni Eneck Thompson ‘Nana Baby’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva anayekuwa kwa kasi nchini Tanzania.

TOLEO NA. 01_OKTOBA 2017

HISTORIA YAKE

Eneck Thompson 'Nana Baby'. Alizaliwa mwaka 1995 jijini Mbeya kwa wazazi Leah na Thompson Mwakibinga. 

Hata hivyo amekulia jijini Dar es Salaam ambako alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Segerea mwaka 2001 na kuhitimu mwaka 2007. Baada ya kufanya vizuri katika masomo yake ya shule ya msingi mwaka 2008 alianza masomo ya upili (sekondari) katika Shule ya Kenton jijini humo na alihitimu mwaka 2011. 

Hata hivyo aliamua kujikita katika muziki wa Bongo Fleva huku akiwa ameanza kutoa nyimbo nne ambazo zitamfanya atoe albamu.

Timothy Ayieko is no more


Shirikisho la Soka la Uganda limetoa salamu zake za rambirambi kutokana na kifo cha aliyekuwa kocha wa zamani wa timu ya Taifa Uganda Cranes Timothy Ayieko. Kocha huyo alifariki jana Jumapili Novemba 19 mwaka huu. 

“Tumepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Timothy Ayieko. Medani ya soka imepoteza mtu mkubwa ambaye alikuwa akipenda soka lianze kutoka chini (grass roots). Alikuwa mchezaji, kocha na mtawala aliyeipenda kazi yake.” 

Ayieko alikuwa kiungo muhimu katika mafanikio ya Uganda Cranes na SC Villa kwa miaka mingi. Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda nyumbani kwake Kakira, Jinja kwa taratibu za mazishi. 

Ayieko alikuwa katika kikosi kilichofanya vizuri mwaka 1978 katika mataifa ya Afrika na kushika nafasi ya pili yakiwa ni mafanikio ya juu kwa timu hiyo ya taifa. 

Aidha aliwahi kuzitumikia KCCA ya Uganda na Gor Mahia ya Kenya  kabla ya kushika mikoba ya Uganda Cranes mwaka 1995. Alizaliwa mwaka 1954.

Thursday, November 16, 2017

Hamad Ndikumana is no more

Hamad Ndikumana enzi za uhai wake
Kumekuwa na mkanganyiko kuhusu Ndikumana miongoni mwa wafuatiliaji wa masuala mbalimbali ya michezo Tanzania na Afrika kwa ujumla. Hiyo inatokana na kifo cha mwanasoka wa zamani wa Rwanda aliyewahi kufanya kazi nchini Tanzania.

Huyo sio mwingine ni Hamad Ndikumana. Mwanasoka huyo ni yule aliyekuwa mume wa muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya. Ndikumana aliwahi kuitumikia klabu ya Stand United ya Shinyanga ambayo ipo katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Nyota huyo amefariki dunia akiwa na miaka 39 kutokana na kile kinachodaiwa kuwa maradhi ya moyo yaliyojificha. Uhusiano wake na Uwoya ulikuwa maarufu mno nchini kutokana na kukutana na misukosuko ya kila mara. Muda mfupi baada ya taarifa za kifo chake, idadi kubwa ya watu katika mitandao ya kijamii walieleza kushitushwa na tukio kila mmoja akieleza la kwake.

Daktari ya klabu ya Rayon Sports, Charles Mugemana alikaririwa akisema Ndikumana hakuwa kulalamika kuhusu tatizo la afya na siku moja kabla ya kifo chake alifanya mazoezi na timu hiyo. 

Taarifa nyingine zilidaiwa kuwa katika eneo alilokuwa akiisha la Nyakabanda, Nyarugenge alimwambia jirani yake yake kuwa ana maumivu makali ya kifua kabla ya kuaga dunia. Ndikumana alikuwa miongoni mwa walinzi bora kuwahi kutokea Rwanda kabla ya kustaafu mwaka 2015.

Alianza kufundisha timu ya mtaani ya Espoir FC. Msimu uliopita alikuwa kocha msaidizi wa Musanze FC akimsaidia Kocha Mkuu Sosethen Habimana ambaye ni mlinzi wa zamani wa Rayon Sports. Hadi mauti yanamkuta alikuwa Kocha msaidizi wa Rayon Sports akisaidiana majukumu na kocha mkuu Olivier Karekezi.

Ndikumana alizikwa Novemba 15, 2017 katika makaburi ya Nyamirambo. Kifo chake kimekuja ikiwa siku moja baada ya mchezaji mwingine wa zamani wa Amavubi Bonaventure ‘Gangi’ Hategekimana kulazwa Hospitali ya Kabutare kutokana na maradhi ya muda mrefu.

 Ndikumana alianza kutambana katika medani ya kandanda baada ya kujiunga na Rayon Sports msimu wa 1998/99.


Aliitumikia timu ya taifa ya Rwanda mitanange 51 huku akiweka rekodi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika nchinio Tunisia mwaka 2004. 
Mwili wa marehemu Hamad Ndikumana ukipelekwa mazikoni.

Tuesday, November 14, 2017

Italia yashindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958

Haitasahaulika Novemba 13, 2017 katika soka la Italia pale timu ya taifa hilo maarufu Azzuri iliposhindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 litakalofanyika nchini Russia.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni miaka 60 ya kuwamo kwenye kila fainali ya Kombe la Dunia. Mabingwa hao mara nne wa taji hilo wakicheza na Sweden katika mchezo ambao uliipeleka Sweden Kombe la Dunia walitoka sare tasa ikiwa ni uwiano wa bao 1-0.
Mlinda mlango ambaye anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa hilo Gianluiggi Buffon alibubujikwa na machozi pale aliposhuhudia kikosi cha miamba hiyo chenye wapenzi na mashabiki wengi ulimwenguni kikishindwa kutinga kwenye fainali hizo.
Italia ilishindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho mwaka 1958. Wakati ule dunia nzima ilikuwa ikimzungumzia Mbrazil Pele lakini fainali za mwaka 2018 Neymar ndiye nyota wa Brazil aliye midomoni mwa wapenzi na  mashabiki wengi.

HISTORIA YA TIMU YA TAIFA YA ITALIA
Nazionale di Calcio Italiana kama ambavyo Waitaliano wenyewe wanavyopenda kuiita Timu ya Taifa ya Italia ipo chini ya Shirikisho la Soka la Italia (FIGC).
Ni miongoni mwa timu zenye mafanikio makubwa ya soka hususani katika Kombe la Dunia  ikitwaa mwaka 1934, 1938, 1982 na 2006 pia ni timu iliyofika kwenye fainali mara mbili mwaka 1970 na 1994. Mwaka 1990 ilishika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia.
Mwaka 1978 ilisalia kushika nafasi ya nne. Mwaka 1934 ilikuwa ni timu ya kwanza kulitetea taji lake. Mwaka 1968 Italia ilitwaa taji la Ulaya ambalo kwa sasa linafahamika kwa jina la Euro.
Pia ilifika fainali mbili Euro 2000 na Euro 2012. Italia ina taji moja la Olimpiki ililotwaa mwaka 1936. Mafanikio makubwa katika Kombe la Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ilikuwa ni nafasi ya tatu mwaka 2013. Italia inayofahamika kwa Gli Azzuri inatumia uwanja wa mazoezi wa Coverciano, Florence yalipo makao makuu ya FIGC.

ITALIA KATIKA KIPINDI CHA 1946-1966
Mwaka 1949 wachezaji 10 kati 11 waliuawa  katika shambulio la anga (Superga Air Disaster) lililotokea Torino ambayo ilikuwa imetwaa mataji matano ya Serie A hivyo Italia haikufanikiwa kufuzu kucheza mzunguko wa pili wa kuwania kucheza Kombe la Dunia la 1950.
Hiyo ilitokana na kudhoofishwa na shambulio hilo. Baada ya hapo timu ikawa inasafiri kwa kutumia boti badala ya ndege ikihofia tukio jingine la anga. Katika kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 1954 na 1962 Azzuri iliishia mzunguko wa kwanza  na haikufuzu kabisa kucheza mwaka 1958.
Italia  haikufanikiwa kuingia katika michuano ya kwanza ya Ulaya mwaka 1960 kwa wakati huo ikiitwa European Nations Cup. Pia katika Euro 1964 iliishia kutolewa katika hatua ya 16 na USSR. Katika kushiriki Kombe la Dunia mwaka 1966 iliishia kuzabuliwa na Korea Kaskazini kwa bao 1-0 licha ya kupewa nafasi.
Kikosi cha Italia kilikuwa na wakali Gianni Rivera na Giacomo Bulgarelli ambao walishindwa kuivusha mzunguko wa kwanza dhidi ya Korea Kaskazini ambao hawakuwa na kiwango cha kuizidi Azzuri. Italia ililaumiwa sana iliporudi katika ardhi ya nyumbani huku mfungaji wa Korea Kaskazini Pak Doo-ik akishangilia kama Daudi kumuuwa Goliathi.

ITALIA YA 1988-2000
Mwaka 1986 aliondoka Kocha Bearzot kisha nafasi yake ikachukuliwa na Azeglio Vicini. Kocha huyo mpya alitoa nafasi kwa vijana chipukizi Ciro Ferrara na Gianluca Vialli. 
Vialli ambaye alikuwa mshambuliaji wa Sampdoria wakati huo alifunga mabao yaliyoipa Italia kufuzu Euro 1988. Alionyesha kuwa ataimudu vema nafasi iliyoachwa na Altobelli ambaye alikuwa na mfanano katika ufungaji wa mabao yake.
Washambuliaji hao wawili waliimaliza Ujerumani licha ya Azzuri kutandikwa na USSR katika nusu fainali. Mwaka 1990 Italia walipata uenyeji wa kuandaa Kombe la Dunia kwa mara ya pili. Wakati huo Azzuri ilikuwa na vipaji katika ushambuliaji Salvatore Schillaci na chipukizi Roberto Baggio.
Licha ya kuwa na majina hayo katika ushindi wao katika mechi zote walizocheza Rome hawakuruhusu kutanguliwa bao katika mechi tano za kwanza wakiishia kupoteza katika nusu fainali wakitandikwa na mabingwa Argentina mjini Naples kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kuwa sare 1-1 hadi muda wa ziada (a.e.t). Schilaci aliipa uongozi katika kipindi cha kwanza na Claudio Canniggia akaisawazishia Argentina kipindi cha pili.
Aldo Serena alikosa mkwaju wa penalti na mkwaju wa Roberto Bonadoni ukiokolewa na mlinda mlango wa Argentina Sergio Goycochea. Hata hivyo Azzuri ilijitahidi na kuizabua England kwa mabao 2-1 ambayo iliwapa nafasi ya tatu mjini Bari. Schillaci alifunga mabao sita katika michuano hiyo na kuwa mfungaji bora. Haikuishia hapo Italia ilishindwa kufuzu kucheza Euro 1992.
Katika Kombe la Dunia mwaka 1994 Italia ilipoteza katika mechi ya ufunguzi ikizabuliwa kwa bao 1-0 na Ireland kwenye dimba la Giants karibu na jiji la New York. Ikaja kushinda kwa 1-0 dhidi ya Norway jijini New York kisha sare ya 1-1 na Mexico kwenye dimba la RFK jijini Washington.
Ilifanikiwa kuvuka kundi E kwa uwiano wa mabao kutokana na timu zote kuwa sawa kwa pointi. Katika hatua ya 16 Italia ilipata ushindi wa mabao 2-1 na Nigeria kwenye dimba la Foxboro karibu na Boston, Baggio akisawazisha na kuongeza moja kwa mkwaju wa penalti katika a.e.t Baggio tena akarudi nyavuni katika robo fainali dhidi ya Hispania mjini Boston kwenye ushindi 2-1.
Mabao mengine mawili Baggio aliyafunga dhidi ya Bulgaria kwenye nusu fainali jijini New York kwenye ushindi wa mabao 2-1. Fainali ilichezwa jijini Los Angeles katika dimba Rose Bowl ambako walifika hatua ya changamoto ya mikwaju ya penalti  ambako walishindwa mbele ya Brazil kwa mikwaju 3-2 huku Baggio akiwa katika dozi ya sindano ya kuzuia maumivu baada ya kupata majeruhi ya nyama za paja kukosa mkwaju wa penalti uliogonga mtambaa panya.
Azzuri ilishindwa kuvuka hatua ya makundi ya Euro 1996. Iliwazabua Russia kwa mabao 2-1 lakini ikapoteza dhidi ya Jamhuri ya Czech kwa matokeo hayo hayo.. Gianfranco Zola alishindwa kuiokoa Italia dhidi ya Ujerumani kwa mkwaju wa penalti hivyo kutoka sare tasa.
Katika kampeni za Kombe la Dunia 1998 Azzuri walitandika England mjini London kwa mara ya pili, huku Zola akifunga bao pekee. Katika fainali za Kombe la Dunia ikairudia tena Italia kuamua nani wa kutwaa taji hilo kwa mikwaju ya penalti ikiwa ni mara ya tatu mfululizo. Kama ilivyokuwa kwa Mazzola na Rivera mwaka 1970 ndivyo ilivyokuwa Alessandro Del Piero na Baggio wakifanya kile kinachoitwa staffeta wakajikuta wakipoteza kwa mikwaju 4-3 baada ya sare tasa a.e.t
Katika michuano hiyo Baggio alifunga mabao mawili hivyo kusalia kuwa mchezaji wa Italia aliyefunga kwenye matoleo matatu tofauti ya Kombe la Dunia. Euro ya mwaka 2000 ilimuibua Francesco Totti. Neema ilikuwa upande wa Italia baada ya kuwatandika wenyeji Uholanzi katika nusu fainali.
Mlinda mlango Francesco Toldo aliokoa mkwaju wa penalti. Totti alijulikana kwa mkwaju wake wa penalti wa staili ya ‘cucchiajo’ yaani kijiko kwa waswahili inafahamika kama ‘kuchopu’. Katika fainali hizo Italia ilimaliza nafasi ya pili baada ya kupoteza dhidi ya Ufaransa kwa mabap 2-1 huku bao la dhahabu  likiwaokoa Les Bleus waliosawazisha sekunde 30 kabla ya muda wa majeruhi dakika ya 93. Baada ya kichapo hicho kocha Dino Zoff aliachia ngazi baada ya kupingwa kwa maneno makali na Rais wa AC Milan wakati huo Silvio Berlusconi.

ZAMA ZA GIAN PIERO VENTURA
Kocha Gian Piero Ventura alipokea mikoba ya Antonio Conte Julai 18, 2016 kwa mkataba wa miaka miwili. Mechi yake ya kwanza ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Ufaransa katika dimba la San Nicola Septemba 1 wakiishia kutandikwa bao 3-1.
Siku nne baadaye alishinda mchezo wake wa kwanza dhidi ya Israel ukiwa ni wa ufunguzi wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia mjini Haifa, Israel kwa ushindi wa mabao 3-1. Italia ilimaliza nafasi ya pili ya kundi G nyuma ya Hispania hivyo kutakiwa kucheza mtoano na Sweden.

Katika mchezo huo ndio umeweka rekodi ya kwanza baada ya miaka 59 huku Giorgio Chiellini, Andrea Barzagli, Daniele De Rossi na nahodha Gianluigi Buffon wakitangaza kustaafu majukumu ya timu ya taifa.

Wednesday, October 25, 2017

Ajibu atazuilika Oktoba 28?

Method Mwanjali na Mzamiru Yassin wakijiuliza namna ya kumnyang'anya mpira Ibrahim Ajibu

Mashabiki wa Simba SC 

Ali Shomary akipambana vikali na Ajibu huku Mwanjali akiwa karibu kutoa msaada kumzuia nyota huyo. Picha zote za Ngao ya Jamii Agosti 2017

Ibrahim Ajibu ndio habari ya mjini kuelekea mechi ya watani wa jadi Oktoba 28 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kama ilivyokuwa katika Ngao ya Jamii Agosti mwaka huu wakati wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18. Ajibu ndiye mchezaji ambaye Simba SC inamwogopa kwa sasa kutokana na kuwa msimu uliopita alikuwa akiitumikia Simba kwa mafanikio makubwa hata kuchukua taji la Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania Bara (ASFC). Hiyo ndiyo sababu hata katika mechi ya ngao ya Jamii alibanwa vya kutosha.

AJIBU ALIBANWA HIVI
Mlinzi wa kati Salim Mbonde alikuwa ngao muhimu ya kumpoteza Ajibu. Ulinzi huo ulikamilika pale Method Mwanjali, Ali Shomari na Mzamiru walipoongezeka na kuziba mianya na njia zote za Ajibu kufanya vile atakavyo. Ulinzi huo ulimpa mlinzi wa kushoto Erasto Nyoni kupata mwanya wa kupanda mbele kushambulia hali iliyowarudisha nyuma Ajibu kwa ajili ya kuzuia hivyo kuchelewa kupanda mbele kwa ajili ya kushambulia.

ITAWEZEKANA OKTOBA 28?
Mbonde alipata majeruhi katika mechi dhidi ya Mtibwa hivyo Yusuf Mlipili na Juuko Murshid walibadili nafasi yake. Ambapo walifanya kazi nzuri katika mchezo dhidi ya Njombe Mji walipotoka kifua mbele kwa mabao 4-0. Mzamiru alipata nafasi ya kupanda mbele huku dimba la chini akimwacha Jonas Mkude. James Kotei hakucheza mchezo huoinawezekana yalikuwa malengo ya Kocha Joseph Omog kumpumzisha raia huyo wa Ghana kwa ajili ya kumdhibiti Ajibu.

NAFASI YA EMMANUEL OKWI

Mshambuliaji wa Simba SC Emmanuel Okwi anaongoza kwa ufungaji kwa sasa katika Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa amepachika wavuni mabao saba (7). Mabao hayo ameyafungia yote katika Uwanja wa Uhuru hivyo anaweza akaendeleza kasi ya kufumania nyavu katika dimba hilo. Hata wachezaji wa Young Africans wanajua kuwa wakifanya makosa mbele ya Okwi itawagharimu. Kila timu imejiweka katika tahadhari kubwa.

McCollister is Back


Uko tayari? Young Africans vs Simba SC Oktoba 28


Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Young Africans na Simba utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kama ilivyotangazwa awali. Hakuna mabadiliko.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio katika mchezo huo kwamba watazamaji watakaohitaji kukaa katika Jukwaa Kuu watalipia Sh 20,000 na Mzunguko ni Sh 10,000.


Young Africans na Simba zinarudi kwa mara ya kwanza kucheza katika dimba la Uhuru baada ya takribani muongo mmoja kupita tangu zianze kutumia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Thursday, October 12, 2017

George Oppong Weah ni nani?

George Oppong Weah

UNAPOLITAMKA jina la George Oppong Weah, basi linakuwa na maana sana katika ardhi ya Afrika hususani mashabiki wa kandanda ambao ni yeye tu hadi sasa makala hii inapoandikwa kutoka katika ardhi yenye nchi 54 kutwaa Tuzo ya Mchezo Bora wa Dunia ambayo kwa sasa imeshikiliwa kwa muda mrefu na wachezaji wawili Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Imekuwaje hadi leo tunataka kujua historia yake ya kandanda na maisha yake ya kila siku? Ni sababu moja tu. Sasa ni Rais wa Taifa la Liberia.

Oktoba 10 mwaka huu wananchi wa Liberia walifanya uchaguzi mkuu nchini humo wa kumchagua Rais wa taifa hilo na taarifa za awali zinaonyesha kuwa Weah aliyetwaa Ballon d’or mwaka 1995 anaongoza dhidi ya mpinzani wake ambaye ni makamu wa Rais wa taifa hilo Joseph Boakai.

Licha ya dosari za hapa na pale Tume ya uchaguzi nchini humo imemtangaza mrithi wa Rais Ellen Johnson Sirleaf kuwa ni George Oppong Weah.

Sirleaf ni rais wa kwanza mwanamke barani Afrika ambaye alishinda uchaguzi wa 2005 kufuatia kipindi cha mpito baada ya vita na baadaye alishinda tena 2011.

Wapigakura milioni 2.1 walioandikishwa walipiga kura zao kumchagua rais kutoka idadi ya wagombea 20, ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja na kuwachagua wabunge 73 wa baraza la wawakilishi.

Iwapo kati ya wagombea hao hakuna atakayefikisha asilimia 50 wagombea wawili waliopata idadi kubwa watachuana tena kwenye duru ya pili itafanyika Novemba 7. Wachambuzi wa mambo wameashiria uwezekano wa uchaguzi huo kwenda duru ya pili.

HISTORIA YA GEORGE WEAH
Baada ya kuisha kwa vita vya pili vya ndani ya Liberia Weah akatangaza nia yake ya kuwania uraisi wa nchi yao katika uchaguzi wa mwaka 2005 akiunganisha chama cha Congress for democratic Change.

Pamoja na kuwa maarufu zaidi nchini Liberia, upinzani ulitumia kampeni zake kumkosoa kwa kukosa elimu ya darasani kama kikwazo cha yeye kuiongoza nchi ukilinganisha na mpinzani wake Ellen Johnson Sirleaf ambae alisoma katika chuo cha Harvard.

Wachambuzi pia wa masuala ya kisiasa nchini Liberia walimzungumzia Weah kama mwanasiasa asiye na uzoefu, huku mama Ellen akiwahi kuwa waziri wa fedha kuanzia miaka ya 1970 huku akifanya kazi katika benk ya dunia.

Weah pia alizua maswali kutokana na awali kupewa uraia wa Ufaransa akiwa Paris Saint Germain (PSG) kama mchezaji. Mahakama ilimuondolea vikwazo hivyo vyote na kumruhusu agombee.

Alitikisa nchi nzima kutokana na umaarufu wake lakini matokeo ya mwisho ya uchaguzi yalimpa ushindi mama Ellen Sirleaf kwa ushindi wa 59.4% dhidi ya 40.6% alizopata Weah.
Matokeo hayo ya uchaguzi yalisababisha vurugu kutoka kwa wafuasi wa Weah ambao hawakuridhishwa na taratibu za uchaguzi pamoja na matokeo.

Lakini baadae wadau wa masuala ya siasa nchini Liberia waliwaomba wafuasi wa Weah wakubali matokeo kwani uchaguzi ulikua halali. Kasha bibi Ellen akatangazwa raisi nchini Liberia. Suala la elimu lilikua ni tata nchini Liberia kutoka kwa upinzani na hata kumfanya ashindwe tena kumzuia bibi Ellen Sirleaf katika uchaguzi wa mwaka 2011. 

Weah akachaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha Congress for Democratic Change.

Weah alizaliwa Oktoba Mosi, 1966 huko Grand Kru, Liberia. Alitangazwa mchezaji bora wa dunia mwaka 1995, huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara tatu. Mwaka 2004 aliandikwa katika orodha ya wachezaji 100 bora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambao bado wanaishi.

George Weah alitua barani Ulaya mwaka 1988 baada ya kusajiliwa na kocha Arsene Wenger, akiifundisha AS Monaco kipindi hicho. “Weah ni kipaji cha ajabu. Sijawahi ona mchezaji akijituma kama yeye uwanjani” alikaririwa kocha wa sasa wa Arsenal ya Uingereza, Wenger

Mwaka 1991 Weah alikua katika kikosi cha Monaco kilichoshinda Kikombe cha Ligi ya Ufaransa. Alijiunga na Paris Saint Germain (1992-1995) akishinda kikombe cha ligi mwaka 1994 na kuwa mfungaji bora wa klabu bingwa Ulaya msimu huo huo wa 1994-1995 akifunga magoli 16 katika mechi 25 alizocheza za Ulaya huku akifunga goli la kustaajabisha dhidi ya Bayern Munich katika michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.

Weah alijiunga na AC Milan mwaka 1995 na kushinda kikombe cha ligi ya Italia 1996 na 1999. Mwaka 1995 alishinda tuzo ya Ballon d’Or na kutangazwa mchezaji bora wa FIFA. Weah akawa mchezaji maarufu zaidi katika kikosi cha Milan baada ya kufunga goli la uwezo binafsi, ‘solo goal’ dhidi ya Verona katika dimba la San Siro akiwapiga chenga wachezaji saba kabla ya kufunga.

Baada ya kuondoka Milan Januari 2000, Weah alijiunga Chesea, Manchester City na Olympique Marseille kwa mafanikio ya haraka, kabla ya kuondoka Marseille mwezi Mei 2001 akielekea Al Jazira FC ya Falme za Kiarabu, ambako alicheza na kustaafu soka lake mwaka 2003.

Pamoja na mafanikio makubwa katika ngazi ya klabu, Weah alishindwa kufanya hayo akiwa na timu ya taifa ya Liberia. Alifanya kila alichoweza katika timu ya taifa katika kucheza, kufundisha na kuiwezesha kifedha lakini akishindwa kuisaidia kufuzu hata mara moja katika fainali za kombe la dunia. Huku wakishindwa kwa pointi moja tu kufuzu katika fainali za kombe la dunia zilizo fanyika 2002.


Weah aliichezea Liberia michezo 60 katika kipindi cha miaka 20 na kufunga magoli 22. Amekua ni mchezaji muhimu wa Liberia huku akiwa kocha kipindi fulani na kuwawezesha kifedha.

Jabir Johnson at Mkalama, Singida on 25 May 2016

Jabir Johnson at Mkalama, Singida on 25 May 2016

Jabir Johnson at Msolwa Sec. School

Jabir Johnson at Msolwa Sec. School
It was 28th May 2016

Jabir Johnson (The Journalist)

Ligi Kuu za Kandanda

Ligi Kuu za Kandanda

Jabir Johnson at BWM Stadium

Jabir Johnson Mking'imle

Jabir Johnson in Dar es Salaam

Jabir Johnson in Dar es Salaam

UCL 2015/16

Cristiano Ronaldo

Lake Victoria source of River Nile

Lake Victoria source of River Nile
Jabir Johnson at source of River Nile, Lake Victoria on May 21, 2016
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

G


website counters

TOPSy KRETTS

Followers